TheHItDotCom

TheHItDotCom
we bring you news to your hand

Tuesday, June 4, 2013

vijue vyuo ambavyo ungependa kuja kusoma ewe kidato cha sita....

CHUO KIKUU DSM SASA CHASHIKA NAFASI YA 6 KWA UBORA HAPA AFRICA......

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) sasa kinakamata nafasi ya sita katika Vyuo Vikuu 100 bora vya Afrika. Orodha kamili iko hapa Chini:2012 World University Ranking | Top 100 Universities in Africa
Source:http://www.4icu.org/topAfrica/

Top 100 Universities and Colleges in Africa by the 4icu.org University Web Ranking
1 University of Cape Town 
South Africa
2 University of South Africa 
South Africa
3 University of Pretoria 
South Africa
4 Universiteit Stellenbosch 
South Africa
5 University of the Witwatersrand 
South Africa
6 University of Dar es Salaam 
Tanzania
 
 
 
 
7 Cairo University 
Egypt
8 University of KwaZulu-Natal 
South Africa
9 The American University in Cairo 
Egypt
10 Makerere University 
Uganda
11 Rhodes University 
South Africa
12 University of the Western Cape 
South Africa
13 Mansoura University 
Egypt
14 University of Johannesburg 
South Africa
15 Université Cheikh Anta Diop 
Senegal
16 Assiut University 
Egypt
17 University of Nairobi 
Kenya
18 Zagazig University 
Egypt
19 University of Botswana 
Botswana
20 Université Mohammed V - Agdal 
Morocco

21 University of Ghana 
Ghana
22 Universiteit van die Vrystaat 
South Africa
23 University of Ibadan 
Nigeria
24 Addis Ababa University 
Ethiopia
25 North-West University 
South Africa

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU (HESLB) YASISITIZA:ZINGATIENI MUDA WA KUOMBA MIKOPO

Mkurugenzi wa Mawasiliamo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Cosmas Mwaisobwa
 
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa msisitizo kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita mwaka huu na kujiunga va vyuo vya elimu ya juu kuanza mara moja na kuzingatia ratiba kuomba mikopo hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliamo wa Bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa, wanafunzi hao wanatakiwa kuanza kujaza fomu za maombi na kusisitiza kuwa siku ya mwisho ya kupokea maombi hayo ni Juni 30 mwaka huu.
“Bodi inasisitiza kuanza mchakato wa kuomba mikopo kwa waliomaliza kidato cha sita na kuzingatia muda uliotolewa kujaza fomu za maombi na kuziwasilisha kwenye ofisi za bodi,” alisema.
Akizungumzia kuhusu wanafunzi wanaoendelea na masomo, Mwaisobwa alisema tayari waombaji 62,758 wamekamilisha taratibu za maombi ya mikopo na kujaza fomu stahiki tangu utaratibu huo ulipozinduliwa rasmi Mei Mosi mwaka huu.
“Hadi sasa mchakato kwa waombaji wa mikopo kwa wa mara ya kwanza na wanafunzi wanaoendelea na masomo unaendelea vizuri ambapo wengi wameweza kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao,” alisema.
Aidha, Bodi ya mikopo imewataka waombaji kuzingatia maelezo yaliyotolewa wakati wa ujazaji wa fomu hizo na kuhakikisha wanakamilisha mchakato huo haraka ili kutoa nafasi kwa bodi kuchambua maombi hayo na kupanga madaraja ya mikopo kwa waombaji.
Katika mwaka wa masomo wa 2012/13, Bodi hiyo iliwapatia mikopo waombaji 94,703, ambao wako katika vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu hapa nchini.