TheHItDotCom

TheHItDotCom
we bring you news to your hand

Thursday, February 13, 2014

Wajumbe wa bunge maalum la katiba watakiwa kuweka mbele maslahi ya taifa.

 Makamu wa rais Dk Mohamed  Gharibu Bilal amefungua kongamano la kitaifa la pili la tafakuri na maridhiano kuelekea kuanza mjadala wa rasimu ya pili katika bunge la katiba akisisitiza wadau kutanguliza utaifa na kuweka pembeni maslahi ya vyama vya siasa.
Akifungua kongamano hilo lililo shirikisha wakilishi na viongozi wa vyama vya siasa nchini,viongozi wa dini pamoja na wadau mbalimbali chini ya uratibu wa kituo cha demokrasia nchini TCD Dk Bilali aliyemwakilisha rais Kikwete amekiri ugumu wa mchakato kutokana na hali halisi ya huruka ndani ya vyama na makundi mengine huku akitaka kutumika kwa busara ili mchakato huo ufanikiwe na wananchi wapate wanachotarajia.
Awali akimkaribisha makamu wa rais mwenyekiti wa kituo cha demokrasia nchini TCD Bw. James Mbatia ambaye ametumia muda mwingi kunukuu vitabu vitakatifu, maneno ya wana falsafa,viogozi mashuhuri pamoja na waasisi mbalimbali duniani kueleza kile alichodai kuepuka mjadala kutekwa na makundi au vyama vya siasa na kupoteza dhamira na maoni ya Watanzania amewataka vyama vya siasa kutambua kuwa hakuna chama chenye hati miliki ya katiba ya nchini.
Katika mada ya kwanza mwenyekiti wa tume ya katiba jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba hakusita kurejea sababu za kuweka muundo wa saerikali tatu ikiwewemo matakwa ya Zanzibar kutaka iwe na mamlaka kamili kama nchini, ukikwaji wa katiba ya sasa kwa masuala ya muungano na mambo kadha ikiwemo madai ya jamuhuri kuvaa kofia ya Utanganyika kuimeza Zanzibar mambo ambayo hayana namna yoyote ya kuyarekebisha nje ya serikali tatu.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa walitoa maoni yao kuhusiana na hotuba za ufunguzi wakieleza umuhimu wa kongamano hilo na wasiwasi wa makundi ya kisiasa kutumia nafasi hiyo vibaya kinyume na matarajio ya watanzania huku katibu mkuu CCM Tanzania bara Bw. Philp Magula akieleza hatua hiyo kuwa ya kuelimishana na badae maamuzi ya wananchi.

No comments:

Post a Comment