TheHItDotCom

TheHItDotCom
we bring you news to your hand

Saturday, June 1, 2013

WENGI WAFAULU KIDATO CHA SITA 2013

waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
BARAZA la Mitihani Nchini (Necta), limetangaza matokeo ya kidato cha sita ambapo asilimia 87.85 wamefaulu huku kundi la shule 20 za mwisho likitawaliwa na shule kongwe nchini na zile za Zanzibar.
Akitangaza matokeo hayo jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde, alisema watahiniwa 50,611 walifanya mtihani huo na kati yao 44,366 sawa na asilimia 87.85, wamefaulu.
Mwaka 2012 wanafunzi waliofaulu mtihani huo walikuwa ni 46,658 sawa na asilimia 87.65.
Watahiniwa wa shule
Dk Msonde alisema kuwa, watahiniwa wa shule waliofaulu ni 40,242 sawa na asilimia 93.92 ya waliofanya mtihani huo.
“Wasichana waliofaulu ni 13,286 sawa na asilimia 95.80 na wavulana 26,956 sawa na asilimia 93.03,” alisema.
Mwaka 2012 watahiniwa 40,775 sawa na asilimia 92.30 walifaulu mtihani huo.
Watahiniwa wa kujitegemea
Alisema kuwa, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo walikuwa ni 7,659 na waliofaulu ni 4,124 sawa na asilimia 53.87. Ufaulu katika kundi hili umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 5,883 sawa na asilimia 64.96 ya wote waliofanya mitihani hiyo.
Ufaulu kwa madaraja
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa, watahiniwa 325 sawa na asilimia 0.76 ya wote waliofanya mtihani huo walipata daraja la kwanza, kati yao wavulana wakiwa ni 188 sawa na asilimia 0.65 na wasichana 137 sawa na asilimia 0.99.
Wanafunzi Bora wazungumzia matokeo
MWANAFUNZI bora wa kwanza kitaifa katika matokeo yaliyorekebishwa ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2012, Said Irando kutoka Shule ya Sekondari Feza ya jijini Dar es Salaam, ameeleza kushangazwa na matokeo hayo kwa kuwa hakuyatarajia.
Mwanafunzi huyo ambaye tayari ameshaanza masomo ya Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Feza, alisema kuwa ingawa alisoma kwa bidii lakini hakudhani kama angeweza kushika nafasi ya kwanza kitaifa na kwamba anamini mafanikio yake kitaaluma yana ‘mkono wa Mungu’.
“Sikutegemea kabisa kuwa mwanafunzi bora, ingawa nilisoma kwa bidii kubwa nia yangu ilikuwa ni kutaka kufaulu tu; Ni Mungu amenisaidia,” alisema Irando.
Alisema kujituma katika masomo, mazingira mazuri ya kusomea na upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia ndiyo yaliyomwezesha kusoma na kufanya vizuri.
Irando ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto watatu, alisema kurekebishwa kwa matokeo ya kidato cha nne kulibadilisha alama za matokeo yake kutoka Daraja la kwanza akiwa na alama tisa hadi saba, zilizomfanya kuwa mwanafunzi bora kitaifa na mwafunzi bora wa kwanza kati ya wavulana kumi bora pia kitaifa.
Mwanafunzi huyo alibainisha kuwa pamoja na wazazi wake kuwa ni wafanyabiashara, yeye anatamani kuwa mhandisi ingawa bado hajajua atakuwa mhandisi katika tasnia gani.
“Natamani sana kuwa mhandisi hiyo ndiyo ndoto yangu ingawa bado sijajua nitakuwa mhandisi wa sekta gani,” alisema Irando.
http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2013/06/Naibu-Katibu-Mkuu-wa-Baraza-la-Mitihani-la-Taifa-NECTA-Dk-Charles-Msonde-akitangaza-matokeo-ya-mtihani-wa-kidato-cha-sita-kwa-mwaka-2013-kwa-waandishi-wa-habari-jijini-Dar-es-Salaam-jana.-Picha-na-Fidelis-Feli.jpg
Irando alisoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi J.K Nyerere ambako alifaulu na kuchaguliwa kujiunga na Sekondari Pugu, lakini wazazi wake waliamua kumpeleka Shule ya Sekondari Feza.
Naye mwanafunzi Joshua Azza kutoka Sekondari ya Wavulana Marian ambaye ameshika nafasi ya saba kitaifa kati ya wanafunzi kumi bora baada ya kupata daraja la kwanza akiwa na alama 11, alisema ameyapokea matokeo hayo kwa furaha akiamini atatimiza lengo lake la kuwa daktari wa upasuaji.
“Natarajia kuwa daktari wa upasuaji, kwa matokeo haya nadhani nitafanikiwa,” alisema Azza ambaye wazazi wake wote ni walimu alipozungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Saidi Nchimbi kutoka Sekondari ya Feza, ambaye ameshika nafasi ya nane kati ya wanafunzi kumi bora kitaifa, alisema kuwa siku zote alikuwa akisoma kwa uwezo wake wote na kwamba alikuwa akitamani kufaulu kwenye mitihani yake yote aliyopewa. Nchimbi amefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kupata daraja la kwanza akiwa na alama nane. Katika matokeo ya awali mwanafunzi huyo alikuwa na alama 11.

No comments:

Post a Comment