Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi -CCM, mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida na wenzake watano wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kusambaza dawa bandia za kurefusha maisha ARV na kuisababishia serikali hasara ya Sh. Milioni 148.3.
Wakili wa serikali Shedrack Kimaro amedai mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu, jijini Dar es Salaam Nyigulila mwaseba kuwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka matano na shtaka la kwanza ni la kusambaza dawa hizo ambapo wanadaiwa Aprili 5, 2011 wakiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam walisambaza dawa hizo katika Bohari ya dawa MSD makopo ya dawa 7776.
Amedai kuwa dawa hizo muda wa kutengenezwa ulikuwa Machi, 2011 na muda wa kuisha ni Februari 2013 katika shtaka la pili wanatuhumiwa kusambaza dawa hizo bandia makopo 4476 MSD, Aprili 11, 2011 wakiwa Dar es Salaam na katika shtaka la tatu Madabida, Shamte, Msofe na Shango wanatuhumiwa kati ya aprili 12 na 29 mwaka 2011 walijipatia shilingi milioni 148.3 kutoka msd, wakijaribu kuonesha kuwa fedha hizo zilikuwa halali kwa malipo.
Wakili kimaro amedai kuwa katika shtaka la nne la uzembe wa kuzuia kufanyika kwa kosa linamkabili materu na mwemezi ambao wote ni wafanyakazi wa msd wanadaiwa kulitenda kosa hilo kati ya aprili 5 na aprili 13, 2011 ambapo washtakiwa hao wakijua kabisa kuwa dawa hizo ni za bandia walishindwa kwa nyadhifa zao kuzuia kitendo hicho kisitendeke.
Na katika shtaka la tano la kuisababishia serikali hasara ya sh. Milioni 148.3 linawakabili washtakiwa wote, ambapo wanadaiwa kati ya aprili 5 na aprili 30, 2011 waliisababishia hasara hiyo, baada ya kusambaza makopo 12252 ya dawa bandia za arv mara baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka hayo walikana kuhusika na tuhuma hizo.
Hakimu mwaseba amesema dhamana iko wazi ambapo washtakiwa wanatakiwa wawe na wadhamini wawili wakuaminika watakao saini bondi ya maneno ya sh. Milioni 6 na kutoa sh. Milioni 12 taslimu mahakamani au mali isiyohamishika yenye thamani ya fedha hiyo ambapo
Baada ya hakimu kusoma masharti hayo, waliyotimiza masharti hayo ni madabida na materu wengine wamepelekwa rumande na kesi hiyo itatajwa februari 24 mwaka huu.
Wakati huo huo aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa wakala wa majengo tanzania (tba), makumba kimweri na msanifu mkuu wake richard maliyaga wameachiwa huru, katika kesi iliyokuwa inawakabili ya kutoa kibali cha jengo refu lililojengwa jirani na ikulu bila kufuata utaratibu na wameachiwa huru, baada ya kulipa faini ya sh. Milioni 15 kila mmoja, baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka matano yaliyokuwa yakiwakikabili.
No comments:
Post a Comment