TheHItDotCom

TheHItDotCom
we bring you news to your hand

Thursday, February 13, 2014

Rais wa TFF aelezea changamoto za siku 100 za uongozi wake.


 Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Gamal Malinzi amesema siku miamoja za uongozi wake katika  shirikisho hilo amekutana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja kukuta madeni mengi pamoja na mikataba isiyokuwa na tija.
Ukisoma kitabu cha pili cha mwandishi Nguli Leroy Brownlow utabaini kuwa mwandishi alitaka kuiaminisha jamii kiongozi anayependwa na umma anaweza kuleweshwa  na upendo huo na akasahau kutekeleza ahadi rais wa TFF Gamali Malinzi akiwa na siku 100 tu ofisini kwake anaweza kusoma kitabu cha Lery Brownlow kama kinamuhusu ama laa kisha akajipima.
Akielezea siku 100 alizokaa katika kiti hicho malizni amesema amefikia malengo alotaraji lakini amekuwa akivutwa shati kurudi nyuma na baadhi ya maswala ikiwa ni pamoja na kukuta madeni mengi  yaliyoachwa na utawala uliyopita.
Malinzi pia amezungumzia udhia wa tiketi za kieletronick huku akijitoa kuwa mtaka huo ameukuta na una kasoro nyingi ingawa ina nia njema.
Siku miamoja za unahodha wake katika jahazi la soka nchini Tanzania pamoja na jitihada za dhahiri anazoonyesha katika kukuza soka nchini pia amekumbwa na kadhia za kudekeza ukabila hasa kanda ya ziwa jambo analolikanusha vikali kama alivyokanusha leo. 

Kongamano la tafakuri kuhusu katiba mpya latoka na maadhimio 16

 Maazimio na kufungwa mkutano wa TCD kongamano la kitaifa la tafakuri na maridhianio kwa wadau wa siasa na maendeleo nchini kuelekea mjadala wa bunge la katiba limefungwa na rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Dk. Aly Mohamed Shein kwa kuazimia maazimio 16 likiwemo mjadala wa bunge la katiba kuongozwa na hoja badala ya msukumo wa makundi ya kisiasa.
Akifunga kongamano hilo rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Dk. Aly Mohamed Shein pamoja na kupongeza maazimio hayo amewahakikishia Watanzania kuwa dhamira yake pamoja na mwasisi wa katiba rais Jakaya Kikwete kuendelea kusimamia maslahi ya taifa bila upendeleo wa aina yoyote kwa mstakabali wa Tanzania kwa miaka mingi ijayo.
Akisoma maazimio hayo 16 mwenyekiti wa kituo cha demokrasia nchini TCD James Mbatia ameyataja kuwa ni pamoja bunge maalumu kuzingatia maslahi ya kitaifa, uwazi pamoja na kuzingatia ushauri wa  kitaalamu kutoka ndani na nje ya nchi na kituo cha demokrasia kuendeleza mijadala ya maridhiano kwa makundi mbalimbali pamoja  na vyombo vya habari nchini kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya  maazimio hayo.
Aidha katika kile kilichoelezwa kuwa ni kuhakikisha maazimio hayo yanazingatiwa TCD imekabidhi nakala kwa vyama vyote vya siasa mahakama,maspika wa bunge la wawakilishi na jamuhuri ya muungano, msajili wa vyama vya siasa, tume ya katiba, taasisi zote za dini, ofisi ya waziri mkuu,kiongozi wa shughuli za serikali baraza la wawakilishi Zanzibar, asasi za kiraia, viongozi mashuhuri.

Wajumbe wa bunge maalum la katiba watakiwa kuweka mbele maslahi ya taifa.

 Makamu wa rais Dk Mohamed  Gharibu Bilal amefungua kongamano la kitaifa la pili la tafakuri na maridhiano kuelekea kuanza mjadala wa rasimu ya pili katika bunge la katiba akisisitiza wadau kutanguliza utaifa na kuweka pembeni maslahi ya vyama vya siasa.
Akifungua kongamano hilo lililo shirikisha wakilishi na viongozi wa vyama vya siasa nchini,viongozi wa dini pamoja na wadau mbalimbali chini ya uratibu wa kituo cha demokrasia nchini TCD Dk Bilali aliyemwakilisha rais Kikwete amekiri ugumu wa mchakato kutokana na hali halisi ya huruka ndani ya vyama na makundi mengine huku akitaka kutumika kwa busara ili mchakato huo ufanikiwe na wananchi wapate wanachotarajia.
Awali akimkaribisha makamu wa rais mwenyekiti wa kituo cha demokrasia nchini TCD Bw. James Mbatia ambaye ametumia muda mwingi kunukuu vitabu vitakatifu, maneno ya wana falsafa,viogozi mashuhuri pamoja na waasisi mbalimbali duniani kueleza kile alichodai kuepuka mjadala kutekwa na makundi au vyama vya siasa na kupoteza dhamira na maoni ya Watanzania amewataka vyama vya siasa kutambua kuwa hakuna chama chenye hati miliki ya katiba ya nchini.
Katika mada ya kwanza mwenyekiti wa tume ya katiba jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba hakusita kurejea sababu za kuweka muundo wa saerikali tatu ikiwewemo matakwa ya Zanzibar kutaka iwe na mamlaka kamili kama nchini, ukikwaji wa katiba ya sasa kwa masuala ya muungano na mambo kadha ikiwemo madai ya jamuhuri kuvaa kofia ya Utanganyika kuimeza Zanzibar mambo ambayo hayana namna yoyote ya kuyarekebisha nje ya serikali tatu.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa walitoa maoni yao kuhusiana na hotuba za ufunguzi wakieleza umuhimu wa kongamano hilo na wasiwasi wa makundi ya kisiasa kutumia nafasi hiyo vibaya kinyume na matarajio ya watanzania huku katibu mkuu CCM Tanzania bara Bw. Philp Magula akieleza hatua hiyo kuwa ya kuelimishana na badae maamuzi ya wananchi.