TheHItDotCom

TheHItDotCom
we bring you news to your hand

Thursday, February 13, 2014

Kongamano la tafakuri kuhusu katiba mpya latoka na maadhimio 16

 Maazimio na kufungwa mkutano wa TCD kongamano la kitaifa la tafakuri na maridhianio kwa wadau wa siasa na maendeleo nchini kuelekea mjadala wa bunge la katiba limefungwa na rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Dk. Aly Mohamed Shein kwa kuazimia maazimio 16 likiwemo mjadala wa bunge la katiba kuongozwa na hoja badala ya msukumo wa makundi ya kisiasa.
Akifunga kongamano hilo rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Dk. Aly Mohamed Shein pamoja na kupongeza maazimio hayo amewahakikishia Watanzania kuwa dhamira yake pamoja na mwasisi wa katiba rais Jakaya Kikwete kuendelea kusimamia maslahi ya taifa bila upendeleo wa aina yoyote kwa mstakabali wa Tanzania kwa miaka mingi ijayo.
Akisoma maazimio hayo 16 mwenyekiti wa kituo cha demokrasia nchini TCD James Mbatia ameyataja kuwa ni pamoja bunge maalumu kuzingatia maslahi ya kitaifa, uwazi pamoja na kuzingatia ushauri wa  kitaalamu kutoka ndani na nje ya nchi na kituo cha demokrasia kuendeleza mijadala ya maridhiano kwa makundi mbalimbali pamoja  na vyombo vya habari nchini kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya  maazimio hayo.
Aidha katika kile kilichoelezwa kuwa ni kuhakikisha maazimio hayo yanazingatiwa TCD imekabidhi nakala kwa vyama vyote vya siasa mahakama,maspika wa bunge la wawakilishi na jamuhuri ya muungano, msajili wa vyama vya siasa, tume ya katiba, taasisi zote za dini, ofisi ya waziri mkuu,kiongozi wa shughuli za serikali baraza la wawakilishi Zanzibar, asasi za kiraia, viongozi mashuhuri.

No comments:

Post a Comment