Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Gamal Malinzi amesema siku miamoja za uongozi wake katika shirikisho hilo amekutana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja kukuta madeni mengi pamoja na mikataba isiyokuwa na tija.
Ukisoma kitabu cha pili cha mwandishi Nguli Leroy Brownlow utabaini kuwa mwandishi alitaka kuiaminisha jamii kiongozi anayependwa na umma anaweza kuleweshwa na upendo huo na akasahau kutekeleza ahadi rais wa TFF Gamali Malinzi akiwa na siku 100 tu ofisini kwake anaweza kusoma kitabu cha Lery Brownlow kama kinamuhusu ama laa kisha akajipima.
Akielezea siku 100 alizokaa katika kiti hicho malizni amesema amefikia malengo alotaraji lakini amekuwa akivutwa shati kurudi nyuma na baadhi ya maswala ikiwa ni pamoja na kukuta madeni mengi yaliyoachwa na utawala uliyopita.
Malinzi pia amezungumzia udhia wa tiketi za kieletronick huku akijitoa kuwa mtaka huo ameukuta na una kasoro nyingi ingawa ina nia njema.
Siku miamoja za unahodha wake katika jahazi la soka nchini Tanzania pamoja na jitihada za dhahiri anazoonyesha katika kukuza soka nchini pia amekumbwa na kadhia za kudekeza ukabila hasa kanda ya ziwa jambo analolikanusha vikali kama alivyokanusha leo.
No comments:
Post a Comment